>

FUNGA KAZI 2023/24, MATOKEO HAYA HAPA

MWISHO wa ubishi imefahamika nani atakuwa nani kwenye kila idara ambapo Yanga mabingwa wa ligi na wanaye mfungaji bora ambaye ni Aziz KI akiwa katupia mabao 21 msimu wa 2023/24.

Simba ngoma imegota mwisho ikiwa nafasi ya tatu huku Geita Gold na Mtibwa Sugar hizi zimeshuka daraja mazima.

Matokeo ya mechi zote ambazo zilikuwa live Azam TV yapo namna hii:-

Simba 2-0 JKT Tanzania (Saido 88’p, Onana 90’+2)

Geita Gold 0-2 Azam (Yeison 58’, Feisal 71’)

Yanga 4-1 TZ Prisons (Aziz Ki 11’, 12’, 79’ Musonda 52’ / Ngassa 5’)

Namungo 3-2 Tabora United (Buswita 19’, 28’p, Manyanya 77’ / Abbas 84’, Moses)

Coastal Union 0-0 KMC

Mashujaa 3-0 Dodoma Jiji (Lusajo 6’, 47’, Ulomi 84’)

Ihefu SC 5-1 Mtibwa Sugar (Bola 5’, Chukwu 16’, Mgunda 41’, 62’, 74’ / Karihe 37’)

Singida FG 2-3 Kagera Sugar mabao yakifungwa na Kidemile dakika ya 19’, Kaseke 84’p / Mafie 40’, Mbaraka 46’, Mhilu 82.

Source: Azam TV.