RAIS CAF AGUSIA BAO LA AZIZ KI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

RAIS wa shirikisho la soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe yupo Tanzania akiwa Visiwani Zanzibar kwenye fainali za African Schools Football ambapo akiwa huko amezungumza na Waandishi wa Habari masuala mengi kuhusu michezo.

Kwenye mazungumzo yake rais huyo amegusia na bao ambalo alifunga kiungo mshambuliaji wa Yanga, Aziz KI kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali ugenini dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusinini.

Rais amekiri kuwa kama angekuwa shabiki angeona bao la Yanga lililokataliwa mwamuzi katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Mamelod Sundowns Afrika Kusini kuwa lilikuwa bao halali.

Rais Motsepe ameyasema hayo alipowasili visiwani Zanzibar katika na amepokelewa na mwenyeji wake Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Wallace Karia.

“Ningekuwa shabiki pia ningeona lile lilikua ni bao ila mimi ni Rais siwezi kucomment chochote naacha mamlaka zenye haki zifanye Kazi yake.

“Baada ya Mechi ya Mamelodi na Yanga kumalizika nilikutana na Rais Karia nilidhani kama ilikuwa ni goli lakini Rais wa CAF hatakiwi kutoa maoni yake tunatakiwa kuheshim kanuni na sheria za soka na VAR.

Bao hilo lilifungwa na kiungo wa Yanga Stephen Aziz Ki ambapo mwamuzi wa kati alilikataa kwa kile alichoamini mpira haukuvuka mstari na mwisho Yanga ikaondolewa katika hatua ya robo fainali.