MWAMBA MGUNDA NA KASI YAKE HUKO UNYAMANI

JUMA Mgunda Kocha Mkuu wa Simba kwenye mechi ambazo amekaa katika benchi akishirikiana na Seleman Matola ndani ya msako wa dakika 90 ameonyesha kasi huko unyamani.

Ipo wazi kwamba Simba inapambana kumaliza nafasi ya pili na mbabe wake mkubwa ni Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Yusuph Dabo zote zina pointi 63 na mechi mbili zimebaki mkononi.

Msako wa pointi 21 ni pointi 17 wamekomba wakipishana na pointi nne pekee uwanjani. Jumla Simba imekusanya pointi 63 ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 28 msimu wa 2023/24.

Hizi hapa mechi za Mgunda pamoja na matokeo yake namna hii:-Namungo 2-2 Simba, Uwanja wa Majaliwa.

Simba 2-0 Mtibwa Sugar, Uwanja wa Azam Complex.

Simba 2-0 Tabora United, Uwanja wa Azam Complex. Azam FC 0-3 Simba, Uwanja wa Mkapa. Kagera Sugar 1-1 Simba, Uwanja wa Kaitaba. Dodoma Jiji 0-1 Simba, Uwanja wa Jamhuri na Simba 4-1 Geita Gold, Uwanja wa Azam Complex.

Kituo kinachofuata kwa Simba ni dhidi ya KMC unatarajiwa kuchezwa Mei 25 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid itakuwa Mei 25 2024.