SIMBA MABINGWA WA MUUNGANO 2024

HATIMAYE mabingwa wapya wa Muungano 2024 ni Simba baada ya kushinda katika mchezo wa fainali dhidi ya Azam FC.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa New Amaan Complex umesoma Simba 1-0 Azam FC.

Bao la ushindi limefungwa na kiungo mkabaji Babacar Sarr dakika ya 77 ya mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

Dakika 45 za mwanzo milango ilikuwa migumu kwa pande zote mbili hivyo Simba inatwaa taji hilo ambalo lilikuwa linapigiwa hesabu pia na Azam FC.

Azam FC imegotea kuwa mshindi wa pili baada ya kuwa washindi kwenye fainali ya pili dhidi ya KMKM mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex.

Simba walitinga hatua ya nusu fainali ya kwanza dhidi ya KVZ ambapo wao walishinda mabao 2-0 na Azam FC ilishinda mabao 5-2 KMKM.