JOB ANAPAMBANA NA YANGA

BEKI wa kazi ngumu Dickson Job tuzo ya beki bora inanukia kwake kwa mara nyingine tena kutokana na ushirikiano mkubwa uliopo katika timu hiyo.

Mbali na Job ambaye ni mchezaji wa kwanza kufunga bao ndani ya Ligi Kuu Bara ilikuwa dhidi ya KMC kuna kitasa kingine kinaitwa Bacca kitampa ushindani mkubwa kujua nani atakuwa nani.

Hivyo Job ana kazi kupambana na nyota mwenzake wa Yanga katika kuwania tuzo ya beki bora ndani ya ligi.

Yanga baada ya kucheza mechi 22 safu yake ya ulinzi ni namba moja kwa kuruhusu mabao machache ambayo ni 12.

Mchezo wao wa 23 uliahirishwa Aprili 23 dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Meja Isamuhyo unatarajiwa kuchezwa leo Aprili 24.

Kuna mabeki wengi ambao wanafanya kazi kubwa katika kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja msimu wa 2023/24 mtaje unayeamini anafanya kazi kubwa.