Skip to content
MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya JKT Tanzania dhidi ya Yanga uliotarajiwa kuchezwa Aprili 23 2024 Uwanja wa Meja Isamuhyo umeahirisha.
Huu ni mchezo wa mzunguko wa pili ambao ulitarajiwa kuchezwa kwa dakika 90 kusaka mshindi ambaye angekomba pointi tatu.
Timu zote mbili zilikuwa zimewasili uwanjani kwa ajili ya mchezo huo wa ligi uliokuwa unasubiriwa kwa shauku na mashabiki wa timu zote mbili.
Kwa mujibu wa Kamwanga Tambwe, kamishina wa mchezo huo amebainisha kuwa siku na tarehe ya mchezo huo itapangwa.