CHEKI RATIBA YA LIGI LEO

LIGI Kuu Tanzania Bara leo Aprili 13 2024 inaendelea kwa timu kusaka pointi tatu ndani ya uwanja baada ya dakika 90.

Wababe Geita Gold watakuwa nyumbani Uwanja wa Nyankumbu kusaka pointi dhidi ya Mtibwa Sugar ambao nao wanazihitaji pia pointi tatu.

Ihefu watawakaribisha Simba, Uwanja wa Liti kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

Tabora United nyumbani Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi dhidi ya JKT Tanzania.

Kagera Sugar watakuwa Uwanja wa Kaitaba kusaka pointi tatu dhidi ya Dodoma Jiji.