SIMBA YAWAFUATA AL AHLY MISRI KAMILI

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa hatua ya robo fainali Simba wamekwea pipa kuelekea Misri kusaka ushindi dhidi ya Al Ahly.

Huo ni mchezo wa robo fainali wa pili unaokweda kukamilisha dakika 180 katika Ligi ya Mabingwa Afrika na mshindi wa jumla anakwenda kutinga hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa robo fainali mkondo wa kwanza ubao ulisoma Simba 0-1 Al Ahly hivyo wenyeji wana mtaji wa ushindi wa ugenini.

Simba wameweka wazi kuwa wanakwenda kupindua meza, ipo wazi kuwa kupindua meza kunahitaji kujitoa kwelikweli.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua kazi kubwa itakuwa ugenini lakini wapo tayari.

“Tunatambua tuna kazi kubwa ya kufanya ugenini lakini tupo tayari kikubwa mashabiki waendeleza dua na wachezaji wapo tayari kwa mchezo wetu,”.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni Mzamiru Yasin, Che Malone, Ayoub Lakred, Ally Salim, Clatous Chama.