ndani YA Aprili 2024 kikosi cha Simba kina mechi tano za nguvu kwa ajili ya kusaka ushindi kitaifa na kimataifa.
Kwenye mechi hizo moja pekee itakuwa ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mchezo mmoja wa Azam Sports Federation na tatu zitakuwa za Ligi Kuu Bara.
Ipo wazi kwamba mechi zake zote hizo itakuwa ugenini kusaka ushindi na itakutana na mtani wa jad Yanga mzunguko wa pili Uwanja wa Mkapa.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly wakiwa Uwanja wa Mkapa walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 hivyo kibarua kikubwa ni kusaka ushindi wa mabao zaidi ya mawili ugenini.
Hii hapa ratiba ya Simba ndani ya Aprili 2024 namna hii:-Aprili 5 Al Ahly v Simba, itakuwa ugenini, robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Aprili 9 Mashujaa v Simba mchezo wa Azam Sports Federation itakuwa ugenini.
Aprili 13 Ihefu v Simba, Ligi Kuu Bara itakuwa ugenini.
Aprili 2024 Yanga v Simba, utapangiwa tarehe pia itakuwa ugenini
Aprili 2024 dhidi ya Namungo utapangiwa tarehe pia itakuwa ugenini