AZAM FC YAPETA MBELE YA ZIMAMOTO

KLABU ya Azam FC kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimamoto waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 baada ya dakika 90 kukamilika.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Azam Complex Azam FC walianza kupata bao la kuongoza ilikuwa dakika ya 10 kupitia kwa mwamba Kipre Junior katika mchezo huo.

Kabla ya mapumziko Hilika dakika ya 28 aliweka usawa kwa Zimamoto na kufanya ubao kusoma Azam FC 1-1 Zimamoto katika dakika 45 za ushindani.

Kipindi cha pili Azam FC walimaliza kazi kwa kupata bao la ushindi dakika ya 59 kupitia kwa kiungo mshambuliaji Nado ambaye alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti.