KAZI imeanza kwa kocha mpya wa Singida Fountain Gate Jamhuri Kihwelo (Julio) kwenye mchezo wa kwanza kukaa benchi ameanza kwa ushindi na kukomba pointi tatu muhimu.
Ikumbukwe kwamba Julio alitambulishwa kuifundisha timu hiyo Machi 13 2024 na kupewa ajenda 10 muhimu ambazo ni mechi za ligi 10, ya kwanza imekamilikabado kete 9 mkononi.
Singida Fountain Gate FC ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani CCM Kirumba, Mwanza Machi 16 2024 ilishuhudia ubao ukisoma Singida Fountain Gate 1-0 Namungo.
Nyota Nicholas Gyan alipachika bao pekee la ushindi kwenye mchezo hio kipindi cha kwanza ilikuwa dakika ya 15 likadumu mpaka mwisho wa mchezo.
Singida Fountain Gate imefikisha pointi 24 baada ya kucheza mechi 21 na kupanda kwenye msimamo wa ligi kutoka nafasi ya 11 hadi nafasi ya saba.
Ni Ramadhan Kayoko ameshuhudiwa akitoa kadi tatu nyekundu kwenye mchezo wa ligi kati ya Singida Fountain Gate dhidi ya Namungo.