Skip to content
MZAWA Wazir Junior anayetimiza majukumu yake ndani ya KMC wakusanya mapato ameandika rekodi yake kwa kuwa na mabao mengi ndani ya ligi.
Junior amefikisha jumla ya mabao 50 aliyofunga kwenye Ligi Kuu tangu aanze kucheza soka la kulipwa.
Junior amefunga mabao huku akiwa amecheza jumla ya mechi 77 kwenye Ligi Kuu tangu akiwa na Toto Afrika ya Mwanza.
Takwimu zake
Toto Afrika- Mechi 13 na mabao 7 (2015-2016)
Toto Afrika- Mechi 17 na mabao 7 (2016-2017)
Azam FC- Mechi 1 hakuna bao (2017-2018)
Biashara United (loan 6 month)- Mechi 6 mabao 3 (2018-2019)
Mbao FC- Mechi 17 mabao 13 (2019-2020)
Yanga SC -Mechi 4 mabao 2 (2020-2021)
Dodoma Jiji (6 month)- Mechi 7 mabao 4 (2021-2022)
KMC- Mechi 3 bao moja (2022-2023)
KMC – Mechi 17 mabao 11 (2023-24) na bado msimu unaendelea ana nafasi ya kufunga zaidi ya hayo ikiwa atapata nafasi a kuzitumia.
Kutoka kwa beki mchawi, guu kubwa, Marco Mzumbe