Home Uncategorized MERIDIANBET YATOA MSAADA ZAHANATI MWENGE

MERIDIANBET YATOA MSAADA ZAHANATI MWENGE

Kampuni ya Meridianbet awamu hii wamefika mwenge jijini Dar-es-salaam katika Zahanati ya Mlalakua na kufanikiwa kutoa msaada wa vifaa vya kutunza takataka katika Zahanati hiyo.

Kurudisha kwenye jamii yake iliyowazunguka ni kawaida kwa Meridianbet na leo wamegeukia moja ya Zahanati zinazopatikana katika eneo la Mwenge inayofahamika kama Mlalakuwa wakitoa msaada wa vifaa vya kutunza takataka (Dustbins) kwajili ya kuimarisha usafi katika Zahanati hiyo.

Meridianbet wamefanya hivo kwakua hospitali ni sehemu ambayo inatoa huduma za kiafya hivo itakua sio jambo la busara kama sehemu ya kutoa huduma za kiafya ikawa sehemu ya kuharibu afya kwasababu ya uchafu, Na ndio maana mabingwa hao wa michezo ya kubashiri wameamua kutoa msaada wa vifaa vya kuhifadhi takataka.

Aidha mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko kutoka Meridianbet Bi. Nancy Ingram alipata wasaa wa kuongea baada ya kutoa msaada wa vifaa hivo “Meridianbet tunajua na tunathamini sana umuhimu wa Utunzaji wa Mazingira hasa hasa katika zahanati, Kama wadau wa utunzaji wa mazingira tutaendelea kuimarisha na kuhamasisha zaidi utunzaji wa mazingira.”

“Pia tunashukuru Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Mlalakuwa na Uongozi wa Zahanati ya Mlalakuwa kuungana na sisi katika zoezi hili nakutuunga mkono katika hili tulilolifanya leo”

Suka mkeka wako kwenye michezo mikali itakayopigwa leo kwenye ligi mbalimbali barani ulaya na dunia kwa ujumla. Machaguo zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini sasa? Ingia meridianbet na ubashiri sasa.`

Mganga Mfawidhi katika Zahanati hiyo ya Mlalakuwa inayopatikana maeneo ya Mwenge Bi. Zamzam Said Omar alipata nafasi ya kuzungumza na kutoa shukrani zake kwa Meridianbet “Kiukweli ningependa kuwashukuru sana Meridianbet kutuchagua sisi Zahanati ya Mlalakuwa kua moja ya Zahanati ambazo zimepata msaada huu, Lakini kubwa zaidi ni sisi tutahakikisha tunaimarisha usafi eneo hili kwani kwa msaada huu mmetupa sisi deni asanteni sana”.

Previous articleWAZIR JUNIOR ANA BALAA HUYO MABAO 50
Next articleMWAMBA HUYU KWA MIKATO YA KIMYA YANGA BALAA