MWAMBA HUYU KWA MIKATO YA KIMYA YANGA BALAA

UKIWEKA kando jina la Khalid Aucho ambaye kwa sasa anapata matibabu baada ya kuumia mwamba mpya anayetembeza mikato ñdani ya Yanga Joseph GUEDE.

Mchezo dhidi ya Geita Gold Machi 14 alicheza faulo nne dakika ya 36, 53, 56 na 72 alikomba dakika 80 nafasi yake ilichukuliwa na Clement Mzize aliyepiga shuti lililolenga lango dakika ya 87.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-0 Geita Gold.

Bao la ushindi kwa Yanga inayoongoza ligi lilifungwa na Aziz KI dakika ya 28 kwa mguu wa kushoto akitumia pasi ya Okra Magic.

Ikumbukwe kwamba katika mchezo huo beki ambaye kazini kwake kuna KAZI Kibwana Shomari alipata maumivu ya enka dakika ya 39 baada ya kugongana na Yusuph Mhilu katika kupambania mpira wa juu.