YANGA KAZINI TENA LIGI KUU BARA

KAZI inaendelea ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo vinara wa ligi na mabingwa watetezi Yanga wanatarajiwa kuwa na kazi ya kusaka pointi tatu dhidi ya Geita Gold.

Migue Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Ni mchezo wa mzunguko wa pili ambao unatarajiwa kuwa na ushindani kwa timu zote mbili ndani ya uwanja kusaka pointi tatu muhimu.

Yanga imetoka kuambulia ushindi kwenye mchezo wake uliopita dhidi ya Ihefu kwa mabao 5-0 hivyo inakutana na Geita Gold ikiwa na ari ya ushindi kwenye mchezo wao uliopita.

Gamondi ameweka wazi kuwa wanawaheshimu wapinzani wao wataingia kwa tahahadhari kupata ushindi muhimu kwenye mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

“Ukiwazungumzia Geita Gold  sio timu ya kubeza kwani  inaleta ushindani na hilo lipo wazi kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri kwenye mchezo ambao tutakuwa nyumbani.

Wachezaji wapo tayari na tunatambua kwamba kila mmoja anahitaji kuona timu inapata pointi tatu muhimu ni kuwa kwenye mwendelezo bora mashabiki wajitokeze kuona burudani,” .

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 2:15 usiku huku viingilio kwa upande wa mzunguko ikiwa ni 5,000.