Home Sports VIDEO: TALIB HILAL, GLOBAL WAWAKUMBUKA YATIMA RAMADHANI

VIDEO: TALIB HILAL, GLOBAL WAWAKUMBUKA YATIMA RAMADHANI

TALIB Hilal mshauri wa Ufundi wa Timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni ambaye alikuwa ni mchezaji wa zamani wa Simba ametoa sadaka kwa makundi maalumu kuelekea mfungo mtukufu wa Ramadhani.

Hii ni mara ya tano kwa kocha huyo wa timu ya taifa ya ufukweni ya Oman kufanya hivyo akiweka wazi kuwa imani ya dini inasema kuwa kama unacho ni muhimu kutoa na unapopata gawana na mwenzako.

Talib amekuwa akishirikiana na Global Publishers katika suala la kuwakumbuka watoto yatima. Na aliongozana na msaidizi wake, Yusuph Abeid, kipa wa zamani wa Pamba ya Mwanza.

Talib ameweka wazi kuwa kinachopatikana japo kidogo tunagawana na kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu atufungulie kila lililo kheri.

Previous articleAGE OF THE GODS SPIN A WIN KASINO BORA
Next articleMWANANYAMALA YAFIKIWA SIKUKUU YA WANAWAKE