Home Sports PUMZIKA KWA AMANI DR WA MPIRA

PUMZIKA KWA AMANI DR WA MPIRA

 KLABU ya Soka ya Azam, imetangaza kifo cha aliyekuwa daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa, kilichotokea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke.

Dkt. Mwankemwa alianza majukumu yake Azam FC, mwaka 2008 na katika kipindi chote cha utendaji wake, amehusika kuwasindikiza wachezaji katika matibabu ya ndani na nje ya nchi.

Mwankemwa aliingia katika udaktari michezoni mwaka 1982 na wakati huo alianza na timu JKT Ruvu.

Ni Februari 27 taarifa ilitolewa kuhusu kutangulia mbele za haki kwa daktari ambaye maisha yake yalikuwa kwenye kuwapa ushauri, matibabu wanafamilia ya mpira hivyo alikuwa ni daktari wa mpira.

Pumzika kwa amani dr wa mpira.

Previous article”NI KOSA KUMLINGANISHA CHAMA na PACOME – KWELI MO DEWJI ASHUKURIWE YANGA KUFUZU” – SALEH JEMBE…
Next articleBOSI SIMBA AMEWACHANA YANGA ISHU YA KUTINGA ROBO FAINALI