TABORA UNITED NGUVU ZAO NI FA SASA

UONGOZI wa Tabora United umeweka wazi kuwa kwa sasa wameanza maandalizi kuelekea mchezo wao wa Azam Sports Federation dhidi ya Nyamongo kutoka Musoma.

Ipo wazi kwamba mchezo uliopita katika Ligi Kuu Bara uliochezwa Februari 19 ubao ulisoma Tabora United 0-0 Azam FC wakagawana pointi mojamoja.

Pointi moja kwa Azam FC imewapa jumla ya pointi 36 wakiwashusha Simba nafasi ya pili na sasa Azam FC ipo nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao a kufunga na kufungwa dhidi ya Simba.

Ofisa Habari wa Tabora United, Christina Mwagala ameweka wazi kuwa kwa sasa wanaanza maandalizi kuelekea mchezo wao dhidi ya Nyamongo.

“Mara baada ya kutoka sare dhidi ya Azam FC, kikosi cha Tabora United  kimeanza maandalizi ya mchezo wa michuano ya Kombe la Azam Sport Federation ASFC dhidi ya Nyamongo kutoka Musoma Mkoani Mara utakaochezwa Februali 22 katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

“Kikosi cha Nyuki wa Tabora kimeanza kujifua ikiwa ni baada ya kutoka kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara dhidi ya Azam uliochezwa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na kumalizika kwa sare ya kutokufungana.

Tabora United chini ya kocha Mkuu Goran Copnovic inafahamu umuhimu wa michuano hiyo jambo ambalo limepelekea kuendelea na maandalizi siku ya leo ili kuweza kufanikisha malengo ya kusonga mbele katika hatua ya 16 bora ya ASFC.

Tumetoka kwenye mchezo wa Ligi kuu ya NBC jana na Azam FC,na hivyo kutokana na uhitaji wa michuano hii, hatujatoa mapumziko kwa wachezaji wetu kwa sababu tunataka kusonga mbele, ASFC ni mchezo wa mtoano hivyo ukifungwa unaaga mashindano, kama Tabora United tunataka kuchukua kombe hili,”.

Tabora United katika hatua ya 32 bora ilimtoa Monduli Cofee ya Mkoani Arusha kwa kuwafunga magoli manne kwa moja ambapo mchezaji Yohana Mkomolwa akifunga magoli matatu na kupiga hatric huku Mosses Msukanywele akifunga goli moja na hivyo kufanikiwa kusonga mbele hatua ya 16 bora.