Home Sports SIMBA YAGAWANA POINTI NA AZAM FC

SIMBA YAGAWANA POINTI NA AZAM FC

UBAO wa Uwanja wa CCM Kirumba umesoma Simba 1-1 Azam FC na mwamuzi wa kati alikuwa ni Ramadhan Kayoko

Ni Prince Dube alianza kufunga dakika ya 14 bao hilo likawekwa usawa na Clatous Chama dakika ya 90 kwa pigo la faulo.

Wanagawana pointi mojamoja huku wakiachwa kwa pointi 7 na vinara Yanga wenye pointi 37 baada ya kucheza mechi 14.

Azam FC inabaki nafasi ya pili pointi 32 huku Simba yenye pointi 30 safu ya ushambuliaji ikiwa inaendelea na ubutu wake uleule wa zama za Jean Baleke.

Previous articleUSHINDI KWA NJIA 100, CHEZA KASINO YA REGAL CROWN 100
Next articleADHABU KUWAKUTA YANGA ISHU YA USHIRIKIANA? ISHU IPO HIVI