KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Alex Song ameweka wazi kuwa wakati anajiunga na Barcelona sehemu ya mkataba uliandikwa kuwa hatokuwa na nafasi ya kucheza mara kwa mara lakini yeye hakujali hasa alipoona atalipwa mshahara mkubwa.
Hivyo nyota huyo kwake kucheza haikuwa kipaumbele zaidi macho ilikuwa ni kwenye noti, mkwanja ambao alikwenda kuuvuna hap.
Alex Song anasema: “Nilikutana na mkurugenzi wa michezo wa Barca na akaniambia sitaweza kucheza michezo mingi. Sikujali, nilijua kuwa sasa nitakuwa milionea. Wakati Barcelona walinipa mkataba na nikaona ni kiasi gani ningepata, sikufikiria mara mbili.”
Song aliondoka Arsenal akiwa na uhakika wa namba huku akiwa kwenye kiwango cha juu akitengeneza asisti karibia kila mchezo, lakini Barca anakutana na benchi mara kwa mara lakini hakujali.