FAINALI AFCON YA WABABE, DR CONGO MWENDO WAMEUMALIZA

MWENDO wameumaliza DR Congo kwa kupoteza dhidi ya Ivory Coast ambao ni wenyeji wa AFCON 2023 kwa ushindi wa bao 1-0.

Bao pekee la ushindi kwa Ivory Coast lilipachikwa kimiani na Sebastien Haller dakika ya 65 likadumu mpaka mwisho wa mchezo huo.

Katika nusu fainali ya kwanza Nigeria walitangulia kutinga hatua ya fainali Kwa ushindi dhidi ya Afrika Kusini.

Ikumbukwe kwamba miamba hiyo ilifungana 1-1 Kwenye msako wa ushindi ni William Troost Ekong alifunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 67 na Teboho Mokoena akifunga dakika ya 90 Kwa Afrika Kusini kwa mkwaju wa penalti.

Katika timu ya DR Congo kuna miamba ambayo inaitambua vema Ligi Kuu Bara na walikuwa na ushindani ikiwa ni Henock Inonga nyota wa Simba na Fiston Mayele aliyekuwa nyota wa Yanga.

Afrika Kusini walitinga nusu fainali Kwa ushindi wa penalti dhidi ya Cape Verde wameondolewa kwa penati 4-2 dhidi ya Nigeria.

Fainali ni Ivory Coast v Nigeria