>

NYOTA WA YANGA BADO MAJANGA

BADO hajawa fiti winga Agustino Okra Magic aliyewahi kucheza ndani ya Simba kabla ya kuibukia ndani ya kikosi cha Yanga msimu wa 2023/24.

Ipo wazi kwamba Okra alipata maumivu kwenye mchezo wake wa kwanza kuvaa uzi wa Yanga katika mechi za ushindani ilikuwa Mapinduzi 2024, Zanzibar.

Hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza mchezo wa kwanza ndani ya Februari 2 ubao wa Uwanja wa Kaitaba uliposoma Kagera Sugar 0-0 Yanga ikiwa ni sare ya kwanza kwa timu hiyo inayotetea ubingwa.

 Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi alisema kuwa atakosa huduma ya Okra kwa muda kutokana na kutorejea kwenye ubora wake kwa wakati huu.

“Okra bado hajawa fiti atakosekana kwenye baadhi ya mechi tunaamini kwamba ni mchezaji mzuri anahitaji muda kupona ili kurejea uwanjani kuendelea kutimiza majukumu yake.

Tunaikosa huduma yake kwa kuwa mchezaji jukumu lake ni kucheza lakini hakuna namna inapotokea anakuwa hayupo basi timu lazima icheza kwakuwa wote tupo kutimiza malengo ya kupata matokeo,”.

Yanga ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 34mchezo wao uliopita waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Azam Complex.