YANGA HAO WAIFUATA KAGERA SUGAR

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga mapema Februari Mosi wameanza safari kueleka Bukoba kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kaitaba Februari 2 2024.

Timu hiyo Januari 30 ilikuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa raundi ya Pili Azam Sports Federation ilikuwa dhidi ya Hausing FC ya Njombe.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 huku nyota Clement Mzize akifunga hat trick ya kwanza ndani ya Yanga kwa 2024.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Maxi Nzengeli, Skudu Makudubela, Metacha Mnata.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo dhidi ya Hausing langoni alianza kipa Aboutwalib Mshery aliyeruhusu bao moja dakika ya 69 kwenye mchezo huo na mfungaji alikuwa ni Tony Jailos.