GUEDE: SIANGALII MTU USONI… ADAI AMEKUJA KIKAZI YANGA, AMTUMIA SALAMU INONGA

MSHAMBULIJAI mpya wa Yanga, Joseph Guede ametamba kwa kuwaonya mabeki wa timu pinzani akiwemo Inonga Baka anayekipiga Simba kwa kusema kuwa amekuja kufanya kazi na wala hatukuwa na huruma nao.

Utambulisho wa nyota huyo ulikuwa gumzo tangu juzi baada ya Yanga kuweka wazi kuwa kutakuwa na sapraiz kwenye mchezo wao dhidi ya Hausing FC wengi wakitabiri kuwa ni wakati umefika wa kumuona straika wao mpya kwa mara ya kwanza Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar.

Yanga katika dirisha dogo imesajili wachezaji watatu ambao ni Shekhan Ibrahim na Augustine Okrah hawa wote walicheza mechi za Mapinduzi Cup huku Guede akionekana kwa mara ya kwanza jana.

Akizungumza na Championi Jumatano, mshambuliaji huyo alisema kuwa, hajaja Tanzania kumuangali mtu usoni kwani amekuja kufanya kazi yake huku ikiwa ni meseji kwa mabeki wa timu pinzani wakiongozwa na Inonga ambaye anakumbukwa kwa bato lake na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele.

“Kwangu niweke wazi simuhofii beki yoyote na wala sitaki kusikia ukimtaja beki yoyote kuwa labda namuhofia na wala nimemfuatilia mimi nachofahamu ni kutakiwa kutimiza wajibu wangu nikiwa kama mshmabuliaji wa Yanga.

“Nikiwa kama mshambuliaji nafahamu ni wazi kuwa natakiwa kuhakikisha kuwa nafunga mabao ya kutosha, nikisema nianze kumhofia beki wa wapinzani sasa itakuwa ni ngumu kwangu kufunga, nikiwa kama straika wao mabeki ndio wanatakiwa kuniogopa mimi,” alisema mshambuliaji huyo.

Guede anakuwa mchezaji wa mwisho kutambulishwa na yanga baada ya Shekhani Ibrahim kuanza na aliyefuatia kuwa ni Augustine Okrah ambao wote kwa pamoja wameshaivaa jezi ya Yanga na kuonekana tofauti na Guede.