Home Sports MWAKINYO ATUMA SALAMU KWA TWAHA

MWAKINYO ATUMA SALAMU KWA TWAHA

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo amefanikiwa kushinda mkanda wa ubingwa wa WBO Afrika kwa kumchapa Mghana, Elvis Ahorga kwa KO ya raundi ya sana katika pambano la raundi kumi kwenye uzani wa super middle ambalo limepigwa New Amaan Complex, Zanzibar.

Mwakinyo ameshinda pambano hilo huku akiweka rekodi za kushinda mkanda wa ubingwa huo kwa mara ya kwanza ambao umekuwa ni ndoto yake ya muda mrefu.

Akizungumza na Kijiwe cha Ndondi, Mwakinyo alisema kuwa ushindi wake ni salamu tosha kwa bondia wa Morogoro ‘Twaha Kiduku’ kwa amekuwa akipiga kelele muda mrefu za kutaka kupigana naye, hivyo amewataka mapromota kuweka mkwanja wa kutosha ili waweze kumaliza ubishi wao.

“Kwanza namshukuru Mungu kwa kuweza kushinda ubingwa huu lakini niwashukuru mashabiki wangu kwa kuweza kuonyesha imani kubwa juu ya licha ya kukosa nafasi kwa kipindi kirefu lakini wameweza kunivumilia wakati wote huo hadi leo hii naweza kuonyesha kile ambacho naamini nimejaliwa kuwa nacho.

“Lakini ushindi huu nataka uwe salamu tosha kwa yule bondia wao wa Morogoro ambaye wanaosema namuogopa, nipo tayari kupanda naye ulingoni wakati wowote, kitu cha msingi ni kwa promota kuzingatia suala fedha tu na siyo jambo lengine nataka nikatoe fundisho ili wengine waache kufikiria kwa urahisi,” alisema Mwakinyo.

Previous articleAMEPEWA JEZI NGUMU MSHAMBULIAJI SIMBA
Next articleUGUMU WA YANGA MWISHO