NASIB Abdul msanii anayepeperusha bendera ya Tanzania kitaifa na Kimataifa wengi wanamtambua kwa jina la Diamond amefichua siri yake na Legend kwenye muziki wa Bongo Fleva Henry Samir wengi wanamtambua kwa jina la Mr Blue.
Diamond ameweka wazi kuwa Blue alikuwa naye bega kwa bega kabla hajatusua kitaifa kwa kumshika mkono hatua kwa hatua akiwa na malengo ya kuona kwamba anafanikisha malengo ya kuwa msanii mkubwa jambo ambalo limetokea kwa wakati huu.
Wote wawili wamefanya kazi ambayo inasumbua kwa sasa inakwenda kwa jina la Mapozi wakiwa na mkali Jay Melody kwenye ngoma hiyo.
Diamond kupitia ukurasa wake wa instagram amedondosha maneno haya: “Bizzy, Rolemode wa Vijana wengi ambao leo hii eti nasi tunaonekana watu.
“Nakumbuka wakati niko Underground nahaso kutoboa, licha ya ukubwa ulionao haukunidharau ulinifanyia wimbo wangu wa kwanza kwa J SILK, tena ulikuja kunichukua na gari yako nyumbani Kariakoo.
“Ukanifundisha namna ya viitikio vya wimbo napaswa kuwa naviandika Vipi… Baadae wakati nataka kushoot video yangu ya wimbo wa KAMWAMBIE ulinisaidia hadi kutafuta Mamodel wa kushoot nao, tena hadi tukiwadanganya kuwa watashoot na wewe ilimradi tu wakubali kushiriki…
“Wakati natoa wimbo wangu wa KAMWAMBIE bila kujali ubize na Ustar ulionao ulinishika mkono na kunipelekea kwa Wadau wa TV na Radio mbalimbali na kuwakabidhi video ya Wimbo wangu tena kwa mikono yako na kuniombea wanipigie ili nami nitoke!!
” Haujaua tu ni kias gani nakuheshim my Brother …Haujajua ni kias gani leo nimefarijika kupata nawe wimbo mkubwa…. It was my all time Dream, and GOD MADE IT TO BECOME TRUE! Nakushkuru sana Kaka,”.