NYOTA YANGA HESABU ZAKE ZIPO HIVI

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Clement Mzize amesema watapambana kufanya vizuri kwenye mechi zao kwa kuwa wapo tayari kuwapa furaha mashabiki na wao kutimiza malengo yao.

Mzize ni miongoni mwa washambuliaji wazawa ambao wamekuwa ni maji kupwa na kujaa ndani ya Yanga licha ya kutopewa nafasi mara kwa mara akiwa kwenye ubora wake hufanya kazi yake kwa umakini.
Ipo wazi kwamba ndani ya ligi kafunga bao moja ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union alitokea benchi akafunga bao hilo la ushindi Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mshambuliaji huyo amesema:”Bado kuna nafasi ya kufanya vizuri na tunaamini kwamba ligi itakaporejea tutaendelea kuwapa furaha mashabiki.

“Maandalizi ambayo tunayafanya yanatupa imani ya kuwa imara kwenye mechi zijazo na tunaamini itakuwa hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.