Skip to content
JURGEN Klopp Kocha Mkuu wa Liverpool ameweka wazi kuwa hatakuwa ndani ya timu hiyo msimu ujao ikiwa ni maamuzi yake mwenyewe.
Taarifa iliyotolewa na Liverpool imeweka wazi kwamba Klopp mwenyewe amesema hataendelea kuwa na timu hiyo baada ya msimu kuisha.
Kocha huyo amesema:”Baada ya msimu kuisha sitaendelea kuwa katika nafasi ambayo nipo sasa ndani ya Liverpool.
“Kuna mengi ambayo tumefanya ndani ya timu kwa ushirikiano mkubwa lakini ni wakati wa mimi kuondoka ndani ya timu,”.