Home Sports VITA YA GAMONDI YANGA IPO HAPA

VITA YA GAMONDI YANGA IPO HAPA

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga hesabu zake kubwa kwa sasa ni kufanya vizuri kwenye mashindano makubwa matatu ambayo wanashiriki baada ya Mapinduzi 2024 kugota mwisho.

Ipo wazi kuwa Yanga iligotea hatua ya robo fainali Mapinduzi 2024 ubingwa ukibaki kwa mara nyingine mbele ya Mlandege waliupata ushindi wa bao 1-0 Simba kwenye mchezo wa fainali iliyochezwa Januari 13 2024.

Gamondi ameweka wazi kuwa vita nyingine uwanjani ya kusaka ushindi inaendelea kwenye Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika na Azam Sports Federation.

 Gamondi amesema kuwa kila mashindano ambayo wanashiriki ni muhimu kufanya vizuri na kikubwa ni kupata ushindi uwanjani.

“Kwenye mashindano ambayo tunashiriki ni muhimu kupata ushindi kwa kuwa kila mchezo tunahitaji kupata matokeo. Wachezaji wanalitambua hilo hivyo tunafanyia kazi makosa yaliyopita ili tuwe imara.

“Makosa yaliyopita tunafanyia kazi sehemu ya mazoezi hilo linatufanya tuzidi kuwa imara kwa kupunguza zaidi makosa kwenye mechi,”.

Previous articleBEKI HUYU BADO YUPO SANA YANGA
Next articleJUICY FRUITS KASINO, KUSANYA BONASI NA USHINDI KIRAHISI