>

BEKI HUYU BADO YUPO SANA YANGA

BEKI wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi bado yupo ndani ya kikosi hicho baada ya kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo. Beki huyo wa kupanda na kushuka alikuwa nje kwa muda baada ya kupata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly ya Misri lakini kwa sasa tayari amesharejea kwenye ubora wake akiendelea na majukumu ndani ya Yanga.