TAIFA STARS KWENYE MIKONO YA MAKOCHA HAWA

KUELEKEA mchezo wa kuwania tiketi ya kutinga hatua ya 16 bora katika Kombe la Mataifa Afrika, Tanzania inatarajiwa kushuka uwanjani kwa mara nyingine dhidi ya Zambia.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Januari 21 baada ya ule wa kwanza kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Morocco.Ni Kocha Hemed Selemani Morocco, anachukua nafasi ya Adel Amrouche na atasaidiwa na Juma Mgunda kwenye kukiongoza kikosi hicho.

Amrouche ambaye ni Kocha Mkuu wa Stars amefungiwa na Caf kuinoa Taifa Stars kwa mechi 8 kwa kuwa anatuhumiwa kusema Morocco inafanya inavyotaka ikiwemo kujipangia hata waamuzi wake huku Caf inaonekana kupoteza nguvu dhidi ya taifa hilo.

Ipo wazi kwamba Morocco ndiye msaidizi wa Amrouche na Mgunda alikuwa mmoja wa makocha wasaidizi katika kikosi hicho.