STAY AWAY FROM THE SUN

UNAWEZA kushangaa kuwa Jua ni tatizo hapa Ivory Coast? Ngoja nikukumbushe kile kisa cha AFCON ya Cameroon. Kama unamkumbuka mwamuzi Janny Sikazwe katika mechi ya Mali dhidi ya Tunisia, alizua mjadala kumaliza mechi kabla ya muda na match kamishna akamtaka kurejea kumalizia zile dk 5, akaanzisha tena mchezo na baada ya hapo akapelekwa hospitali.

Ishu ilikuwa ukali wa jua na katika nchi za Afrika Magharibi hasa kwenye ukanda wa pwani zina joto kali sana na zaidi si ukali wa jua tu bali unyevunyevu yaani humidity.
Sikazwe aliomba mwamuzi wa akiba amalizie mchezo kwa kuwa alianza kujisikia vibaya na pumzi zinabana. Timu zikaambiwa, Mali wakakubali wakiwa wanaongoza 1-0, Tunisia wakakataa…Ikabidi aendelee na mwisho ndio kikatokea kile kituko.
Sasa hapa Ivory Coast kumekuwa na maonyo uwanjani kutokana na humidity kuwa 76% au zaidi.

Wachezaji pia wamekuwa wakilalamika kutokana na hali hiyo lakini hii ni Afcon ni lazima iendelee.