Home Sports FAINALI YA MAPINDUZI KUWAKUTANISHA WABABE WA PENALTI

FAINALI YA MAPINDUZI KUWAKUTANISHA WABABE WA PENALTI

FAINALI ya Mapinduzi 2024 inawakutanisha wote walioshinda kwa mikwaju ya penalti huku timu inayopoteza ikipeleka malalamiko kwa waamuzi.

Ni Januari 13 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwa wababe wawili waliopata zali la kushindwa kwa mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 ngoma kuwa nzito kwa timu zote mbili.

Ni Mlandege 0-0 APR FC ilikuwa Januari 9 2024 katika penalti ikawa Mlandege 4-2 APR FC ya Rwanda.

Januari 10 Singida Fountain Gate 1-1 Simba, Elvis Rupia kamba mapema dakika ya 11 na Fabrice Ngoma bao dakika 90+8.

Kwenye penalti Singida Fountain Gate 2-3 Simba. Bao la Elvis Rupia dakika ya 11 lilikuwa ni la mapema kwenye mchezo huo na liliwekwa usawa na Fabrince Ngoma dakika ya 90+8.

Ni Ally Salim aliokoa penalti tatu kwenye mchezo huo huku Parapanda akiokoa penalti moja na Ntibanzokiza Saido alikosa.

Previous articleYANGA: SISI BADO TUPO
Next articleALI KAMWE: TUTAREJEA TUKIWA IMARA