FULANA ya Meddie Kagere mshambuliaji wa zamani wa Simba na Gor Mahia imezua gumzo kutokana na ujumbe wake ambao uliandikwa wakati akishangilia.
Ni kwenye Mapinduzi Cup 2023 ambapo mambo yanazidi kuwa katika ubora baada ya wanafainali 2022 kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya JKU SC.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma JKU SC 1-4 Singida Fountain Gate ambapo mabao yaliyopatikana jumla ilikuwa matano.
Saleh Masoud alipachika bao kwa JKU dakika ya 61 kwa mkwaju wa penalti na Elvis Rupia alipachika mabao mawili kwa Singida Fountain Gate ilikuwa dakika ya 16 na 48, Meddie Kagere bao moja dakika ya 80 na Francy Kazadi bao moja dakika ya 86.
Ujumbe wa Kagere kwenye fulana yake ulikuwa unasema :”Ukishamjua mnafki, ishi nae kinafki,”.