GAMONDI AWAPA MALEKEZO MAPYA NYOTA WAKE

MIGUEL Gamondi Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wote ni muhimu kuongeza juhudi kwenye mechi ambazo wanacheza ili kupata matokeo.

Timu hiyo kwenye msimamo ni namba mbili na funga 2023 ilikuwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma baada ya dakika 90 ubao ulisoma Tabora United 0-1 Yanga na bao likifungwa na Aziz KI.

Aziz KI anafikisha mabao 10 akiwa ni namba moja kwa utupiaji ndani ya kikosi cha Yanga pamoja na ligi kiujumla akifuatiwa na Jean Baleke wa Simba na Feisal Salum wa Yanga hawa wana mabao 8.

Gamondi amesema:”Muhimu kwa kila mchezaji kutimiza majukumu yake na kushirikiana kwenye kila mchezo kupata matokeo.

“Tunahitaji kuona timu inaendelea kuwa na ubora kwenye mechi ambazo tunacheza na inawezekana kwa kuwa wachezaji wapo na wanapenda kuona ushindi unapatikana,”.

Yanga inashiriki Mapinduzi Cup ambapo mchezo wake wa kwanza unatarajiwa kuchezwa Desemba 31.