JKT TANZANIA SIO KINYONGE KUFANYA KWELI

BENCHI la ufundi la JKT Tanzania limeweka wazi kuwa palipo na mapungufu watafanyia maboresho kwenye usajili katika dirisha dogo ili kuwa imara zaidi.

Desemba 18 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma JKT Tanzania 0-1 Coastal Union walipoyeyusha pointi tatu wakiwa nyumbani.

Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Malale Hamsini amesema kuwa ushindani kwenye ligi ni mkubwa na kuna makosa ambayo walifanya katika mechi zilizopita hivyo maboresho yanahitajika.

Katika dirisha dogo tunaamini tutalitumia kufanya maboresho kwenye kikosi kwa kuwa kuna sehemu ambazo zinaonekana hazijawa imara hivyo ni muhimu kufanyia kazi hilo,”.

“Kwenye mchezo wa mpira kuna makosa ambayo yanafanyika hayo yanahitaji kufanyiwa maboresho. Kwa mchezaji yeye kazi yake ni kutimiza majukumu yake uwanjani na benchi la ufundi ni kutoa malekezo. Hivyo tutafanyia kazi yale yaliyopita,” .

JKT Tanzania ni nafasi ya 11 kwenye msimamo ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 14.