HAKUNA MBABE, UFUNGUZI WA AMAAN COMPLEX WAFANA

RASMI Uwanja wa Amaan Complex umefanyika baada ya maboresho makubwa yaliyofanywa katika kuboresha uwanja huo ambao kwa sasa unaingia kwenye hadhi nyingine.

Kwenye uzinduzi huo ambao ulikuwa ni wa kihistoria wengi walihudhuria kushuhudia na wengine kutazama mubashara kupitia Azam TV.

Burudani mbalimbali zilifanyika ikiwa ni pamoja na mchezo maalumu wa ufunguzi wa Uwanja wa Amaan Complex, uliochezwa Unguja  Desemba 27 kati ya Zanzibar Heroes na Kilimanjaro Stars.

Mchezo huo dakika 45 za mwanzo ngoma ilikuwa ngumu kwa timu zote na hata dakika 45 za ngwe ya pili ngoma ilikuwa nzito na mwisho ubao ukasoma 0-0..

Burudani pia kutoka kwa wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Diamond, Malkia wa Mipasho Tanzania, Khadija Omar Kopa.

Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi alikuwa mgeni rasmi ambaye aliweka wazi kuwa  “Ile AFCON ile hatutaki ichezwe hapa peke yake tunataka uwanja mpya kama Old Trafford,” .