KASI ya Azam FC kwenye kukomba pointi tatu ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 weka mbali na watoto kutokana na kuendeleza ushindi kila wanaposhuka uwanjani.
Ikumbukwe kwamba baada ya kucheza mechi 13 ni mechi mbili pekee ilipoteza ilikuwa dhidi ya Yanga Uwanja wa Mkapa na dhidi ya Namungo, Uwanja wa Mkapa na ilipata ushindi kwenye mechi 10 na sare mchezo mmoja.
Desemba 21 ikiwa ugenini ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Kaitaba ukisoma Kagera Sugar 0-4 Azam FC huku mkali wao wa kucheka na nyavu akiwa ni Feisal Salum mwenye mabao 8 kibindoni.
Azam FC ni namba moja kwenye msimamo ikiwa na pointi 31 safu yake ya ushambuliaji kibindoni ina mabao 35.
Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kasi yao itaendelea kutokana na uwepo wa wachezaji wenye ubora pamoja na benchi bora la ufundi.
“Kila mchezaji anatambua kazi kubwa inahitajika kufanyika na wakati uliopo ni sasa kuendelea kupambana kupata matokeo chanya na inawezekana kutokana na benchi kuendelea kutoa mbinu kwa wachezaji,”..