Home Sports YANGA YAIPIGIA HESABU MTIBWA SUGAR

YANGA YAIPIGIA HESABU MTIBWA SUGAR

KOCHA Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameweka wazi kuwa hesabu kubwa kwa sasa ni kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Mtibwa Sugar.

Ipo wazi kwamba baada ya kukamilisha mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana kituo kinachofuata ni Azam Complex kuvaana na Mtibwa Sugar.

Huo ni ni mchezo wa ligi unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kupambania pointi tatu.

Ikumbukwe kwamba mwendo wa Mtibwa Sugar haujawa kwenye ubora ikiwa ina pointi tano kibindoni ipo nafasi ya 16 kwenye msimamo huku Yanga ikiwa na pointi 24 nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 9.

Gamondi amesema: “Kila mchezo ambao tunacheza ni muhimu kuona tunapata pointi tatu hivyo kuelekea mchezo wetu ujao wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar tunahitaji pointi tatu,”.

Previous articleCHEZA KASINO YA MTANDAONI LEO UINGIE KWENYE MGAO WA TSH BIL 2
Next articleSIMBA YATAJA MAMBO MATATU KUIKABILI KAGERA SUGAR