AHMED Ally Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa bado kuna nafasi ya timu hiyo kutinga hatua ya robo fainali licha ya matokeo ambayo hayajawa mazuri kwao.
Kwenye mechi tatu ambazo Simba imecheza hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika imeambulia pointi mbili ikipoteza mchezo mmoja jambo ambalo linaongeza ugumu kwa timu hiyo kutinga hatua ya makundi kutokana na ushindani uliopo.
Ally ameweka wazi kuwa njia pekee itakayofungua njia kwao kutusua katika hatua hiyo ni kushinda mechi zao watakazocheza na wataanza Desemba 19 dhidi ya Wydad Casablanca, Uwanja wa Mkapa.