KWA kitendo cha kukataa penalti wakamalia wakerwa na CR 7 wakiambulia makasiriko baada ya mkeka kuchanika kwenye mchezo huo ambao wengi waliamini timu ya mwamba huyo itashida.
Cristiano Ronaldo, mshambuliaji wa Al Nassr FC juzi aliwashangaza watu kutokana na tukio lake la kukataa penalti.
Timu yake ilipata penalti baada ya nyota huyo kufanyiwa faulo ndani ya 18.
Mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Asia uliowakutanisha Al Nassr dhidi ya Iran Persepolis na uliisha ngoma kuwa 0-0.
Ronaldo alionekana akianguka mbele ya mchezaji wa Iran Persepolis na mwamuzi aliamuru penalti ajabu Ronaldo alimfuata na kumwambia sio penalti.
Ikabidi mwamuzi kukiridhisha kwenye VAR ambapo ilionyesha kuwa kweli haikuwa penalti jambo lilionekana kuwakera wacheza mkeka waliamini Al Nassr itashinda.