>

AZAM FC WAKIMBIZA DAKIKA 270

NDANI ya dakika 270 kwenye mechi tatu za ligi, Azam FC wamekimbiza kwa kukomba pointi zote tisa walizokuwa wakisaka ndani ya uwanja.

Chini ya Kocha Mkuu, Yusuph Dabo kwenye mechi tatu mfululizo ilikuwa ni kicheko kwao huku maumivu yakiwa kwa wapinzani wao.

Ilianza na kete ya ugenini ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma ulisoma Mashujaa 0-3 Azam FC, Uwanja wa Highland Estate, Ihefu 1-3 Azam FC na Azam FC 5-0 Mtibwa Sugar.

Kwenye mechi hizo tatu safu ya ushambuliaji ilikusanya mabao 11 huku ile ya ulinzi ikitunguliwa bao moja pekee ndani ya dakika 270.

Mkali wa kucheka na nyavu ni Feisal Salum ambaye kafikisha jumla ya mabao sita kibindoni. Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Kipre Junior alitupia hat trick na bao.Pointi 22 wanafikisha Azam FC kwenye msimamo.