>

SIMBA: KIMATAIFA TUTAWAFURAHISHA

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa watawafurahisha mashabiki watakaojitokeza kushuhudia mchezo wao dhidi ya ASEC Mimosas pamoja na wale watakaokuwa nyumbani.

Ipo wazi kwamba Novemba 25 Simba itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

 Ally amesema kuwa wana kibarua kizito kwenye mchezo wao wa kimataifa lakini mipango yao ni kuwapa furaha mashabiki kwa kutoa burudani na ushindi mzuri.

Tumetoka kwenye mechi ambazo zilikuwa ngumu na matokeo hayakuwa rafiki kwetu. Sasa kuelekea mchezo wetu dhidi ya ASEC Mimosas tutawafurahisha Wanasimba wote kwa kupata ushindi.

“Ni mchezo muhimu kwa kila mmoja, wachezaji wanalitambua na maandalizi yanaendelea hivyo ambacho kipo ni utayari na mashabiki kuzidi kushikamana katika hilo,” alisema Ally.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo katika kikosi cha Simba ni pamoja na Luis Miquissone, Jean Baleke, Moses Phiri hawa wapo fiti huku Aishi Manula akiwa bado hajatengamaa.