>

AZAM FC YAKOMBA POINTI, FEI ATUPIA

KIUNGO wa Azam FC, Feisal Salum amefikisha mabao sita ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kuongeza akaunti yake ya mabao.

Bao hilo alifunga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara walipocheza dhidi ya Mtibwa Sugar.

Ilikuwa ni siku mbaya kazini kwa Mtibwa Sugar abaada ya kuyeyusha pointi tatu ugenini na kichapo kikubwa wakapokea.

Novemba 24 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 5-0 Mtibwa Sugar.

Mabao matatu yalifungwa na Kipre aliyesepa na mpira wake huku Lusajo akitupia bao moja na Feisal Salum moja.

Anakuwa ni kinara kwa utupiaji ndani ya Azam FC ambayo inajikita nafasi ya pili na pointi 22 kibindoni.