SIMBA NA AKILI NYINGINE KIMATAIFA

DANIEL Cadena, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba amesema akili za wachezaji zipo tofauti kabisa na michezo miwili iliyopita.

Simba Novemba 25 ina kibarua çha kusaka ushindi dhidi ya ASEC Mimosas ikiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

Mechi mbili za ligi iliambulia pointi moja na kupoteza tano kwenye msako wa pointi sita ikifungwa dhidi ya Yanga na kuambulia Sare dhidi ya Namungo FC.

Kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, Novemba 5 2023 ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga na kutokana na matokeo hayo yalikuwa sababu ya Simba kusitisha mkataba wao dhidi ya Roberto Oliveira aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

Cadena amesema: “Ni mchezo mgumu ambao utakuwa na ushindani mkubwa lakini tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wetu.

“Akili za wachezaji kwenye mchezo wetu huu ni tofauti na zile za mechi mbili zilizopita. Ambacho tunahitaji ni kufanya vizuri mashabiki wajitokeze,”.