Home Sports YANGA YAZITAKA POINTI TATU ZA WAARABU KIMATAIFA

YANGA YAZITAKA POINTI TATU ZA WAARABU KIMATAIFA

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi wanahitaji kupata pointi tatu za Waarabu wa Algeria, CR Belouizdad licha ya kuwa ugenini.

Timu hiyo inakibarua cha kuanza kusaka ushindi kwenye mchezo wa hatua ya makundi leo Novemba 24 kisha.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 2 usiku kwa saa za Algeria huku kwa Bongo ikiwa ni saa 4 usiku na wakimaliza kazi hiyo watarejea Dar kumenyana na Al Ahly Desemba 2.

 Gamondi amesema kuwa kila mchezo ni muhimu kupata ushinda hasa kwenye mechi za kimataifa ambazo ushindani wake huwa mkubwa.

“Kuna umuhimu mkubwa kupata pointi tatu kwenye mechi ambazo tunacheza katika hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tupo tayari na tunawaheshimu wapinzani wetu, wachezaji wapo tayari na tumewapa maelekezo ambayo yatatuongoza kwenye kutafuta matokeo chanya,” amesema Gamondi.

Kikosi cha Yanga baada ya kuwasili Algeria Novemba 23 walifanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa 5 July 1962 kwa ajili ya mchezo wa leo.

Previous articleSIMBA NA AKILI NYINGINE KIMATAIFA
Next articleWAKIWA ALGERIA, YANGA WASAHAU HABARI ZA USM ALGER