>

STARS YAANZA KAZI, KITUO KINACHOFUATA KWA MKAPA

CHINI ya Kocha Mkuu Adel Amrouche timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliwaduwaza wenyeji wao Niger kwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026.

 Mchezo huo uliochezwa jijini Marrakech, Morocco baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Marrakech Annex One ulisoma Niger 0-1 Tanzania.

Bao pekee la ushindi kwenye mchezo huo lilijazwa kimiani na Charles M’mombwa dakika ya 57 akitumia pasi ya nahodha Mbwana Samatta kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Nyota huyo aliyefunga bao la ushindi kwenye mchezo huo ameweka wazi kuwa furaha yake ni kubwa kwa kufunga kwenye mchezo huo muhimu ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

“Furaha yetu ni kubwa na nimefurahi kufunga kwenye mchezo huu muhimu. Imani yetu ni kuendelea kufanya vizuri kwa mechi zinazofuata na tutapambana kufanya vizuri.

Mashabiki nguvu yao ni kubwa na wamekuwa pamoja nasi hilo linatuongezea nguvu kwenye upambanaji. Kwenye wakati wetu tunaendelea kupambana kufanya vizuri zaidi,”.

Baada ya kuvuna pointi tatu kwenye mchezo huo Taifa Stars imerejea Tanzania kwa ndege iliyotolewa na Rais Samia Suluhu kwa ajili ya kuanza maandalizi kuikabili Morocco mchezo unaotarajiwa kuchezwa Novemba 21 katika Uwanja wa Mkapa.

Kocha Mkuu wa Stars Amrouche ameweka wazi kuwa kikubwa ambacho anakitarajia kwenye mechi zote ni kupata ushindi na kutoa burudani.

“Mchezo wa mpira unahitaji matokeo na kufurahia kile ambacho kinafanywa na wachezaji kwa kutoa burudani. Ninawapongeza wachezaji kwa namna wanavyojituma na kutimiza majukumu yao hilo litaendelea kwenye mechi zetu zote,”.

Ni Aishi Manula alikuwa langoni kwenye mchezo huo dhidi ya Niger ugenini baada ya kuwa nje kwa muda akipambania hali yake na sasa amerejea kwenye majukumu yake ya kazi.

Mbali na Manula nyota wengine waliokuwa kwenye mchezo huo ni pamoja na Bakari Mwamnyeto, Simon Msuva, Feisal Salum

ReplyForward