NYOTA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wameweka wazi kuwa watapambana kupata matokeo kwenye mchezo wao dhidi ya Niger ambao ni wa kufuzu Kombe la Dunia.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Novemba 18 katika Mji wa Marrakech siku ya Jumamosi.
Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni Simon Msuva, Novatus Dismas, Peter Banda, Aishi Manula, Dickson Job, Mbwana Samatta.