Home Sports KOCHA MBABE WA YANGA ATAJWA SIMBA

KOCHA MBABE WA YANGA ATAJWA SIMBA

ABDELHAK Benchikha aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa USM Alger anatajwa kuwa katika hesabu za kupewa mikoba ya Robert Oliveira.

Baada ya ubao wa Uwanja wa Mkapa Novemba 5 2023 kusoma Simba 1-5 Yanga, Novemba 8 Simba ilitangaza kupeana mkono wa asante na Oliveira.

Taarifa zimeeleza kuwa upo uwezekano koçha huyo aliyetwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho mbele ya Yanga akasaini dili la miaka miwili.

Mbali na kocha huyo pia jina la Sven Vandebroeck raia wa Ubelgiji nalo lipo katika orodha ya makocha wanaotajwa kuibukia Simba.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa mchakato wa kumtafuta kocha mpya umefika hatua nzuri na wakati ukifika atatambulishwa.

“Kila kitu kinakwenda sawa na mpango wa kumpata kocha mpya unaendelea wakati ukifika atatambulishwa ni suala la muda tu,”.

Previous articleMESSI, RONALDO, NANI MBABE WA KUAMUA MECHI UWANJANI?
Next articlePICHA: TAIFA STARS YAONDOKA KWENDA MOROCCO KUKIWASHA NA NIGER MCHEZO WA KUFUZU KOMBE LA DUNIA