KISA MGHANA HUYU SINGIDA FOUNTAIN GATE YAPIGWA PINI

IKIWA ni muda wa mapumziko kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara, Klabu ya Singida Fountain Gate inayotumia Uwanja wa Liti imepigwa pini kwenye suala la usajili.

Timu hiyo ya Singida Fountain Gate inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC ya Singida Fountain Gate FC zamani ilikuwa ikiitwa Singida Big Stars FC imefungiwa kusajili mpaka itakapomlipa mchezaji wake.

Uamuzi huo umefanywa na shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya mchezaji Nicholas Gyan kushinda kesi za madai dhidi ya Klabu hiyo.

Klabu iyo imetakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.

Wakati FIFA imeifungia Klabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.

TFF inazikumbusha Klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.